Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Nabii Isaya anarudisha ujumbe kwa mfalme Hezekia kutoka kwa Mungu. Ujumbe unaonyesha kwa undani kabisa jinsi Mungu alivyoona na kusikia yale ambayo Mfalme Senakeribu amefanya. Ni Mungu mwenyewe aliyemwezesha mfalme, kama anavyomwambia katika m.25-26:Je! Hukusikia wewe ya kuwa mimi ndimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale? Sasa mimi nimelitimiza jambo hili, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, hata ikawe chungu na magofu. Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva. Lakini kwa sababu ya kiburi cha mfalme na shutuma zake juu ya Bwana, Mungu atamrudisha njia aliyoijia, hataingia Yerusalemu, na hatimaye atakufa:Njia ile ile aliyojia, kwa njia iyo hiyo atarudi zake, wala hataingia ndani ya mji huu, asema Bwana. Maana nitaulinda mji huu, niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu. Ikawa usiku uo huo malaika wa Bwana alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia. Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akaondoka, akaenda zake, akarudi akakaa Ninawi. Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake(m.33-37).Wayuda wataokolewa na kulindwa na Mungu mwenyewe, maana mabaki yatatoka katika Yerusalemu, na wao watakaookoka katika mlima wa Sayuni, wivu wa Bwana utatimiza jambo hilo. ...Maana nitaulinda mji huu, niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu(m.31, 34). Mungu ni kimbilio na nguvu wakati wa shida.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz