Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Mfalme Hezekia aliposikia jinsi mfalme wa Ashuru alivyomtukana Mungu aliingiwa na jazba nzuri. Alijinyenyekesha, akararua nguo zake na kuvaa magunia, akaingia nyumbani mwa BWANA na kuomba ushauri kutoka kwa nabii Isaya (m.2). Nabii alituma ujumbe wa kumwondoa wasiwasi Mfalme Hezekia kwamba asiogope, kwani matusi wanayopata watumishi wa Mungu ni matusi kwa Mungu mwenyewe. Kwa hiyo, siyo vizuri kujibishana. Badala yake, ni vizuri kukumbuka kwamba Mungu anasikia, na anangojea tu tumhusishe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz