Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
Unafanyaje ukipata matatizo? Angalia mkakati aliokuwa nao mfalme Hezekia: Aliwaonya watu wake wasijibishane.Watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana amri ya mfalme ilikuwa kwamba, Msimjibu neno(18:36). Alijidhili, akaingia nyumbani mwa BWANA na kumshirikisha nabii Isaya:Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya Bwana. Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wamevikwa nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi(19:1-2). Kisha, alipoingia madhabahuni (m.14), akauweka waraka mbele za Bwana, akamwomba akimsifu kwa ukuu na uweza wake,akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi(m.15). Alimwomba Mungu aone na asikie matusi aliyoletewa Mfalme: Tega sikio lako, Ee Bwana, usikie; fumbua macho yako, Ee Bwana, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, ambayo amemtuma mtu aje nayo ili kumtukana Mungu aliye hai(m.16). Aliomba Mungu awaokoe ili ulimwengu ujue kwamba Yeye ndiye Mungu wa kweli. Tunapopata matatizo tufanye kama Hezekia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz