Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Mfalme Hezekia aliugua sana. Mungu alimtuma nabii Isaya kumwambia mfalme ajiandae kufa, hatapona, kwani ugonjwa alio nao ni wa mauti. Tena Hezekia anajua pa kukimbilia. Anamsihi Mungu kwa machozi mengi akilia sana sana:Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako(m.3). Tujiulize: Je, tunamkimbilia nani wakati wa magumu? Maombi yetu yakoje? Tuna ujasiri wa kumkumbusha BWANA juu ya kuishikatika kweli? Kwamoyo mkamilifu? Na katikakutenda yaliyo mema? Mungu anasikia maombi na kumrudisha Isaya kwa Hezekia na taarifa za kupona na kuongezewa miaka 15.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 11/2024](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F52667%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz