Soma Biblia Kila Siku 11/2024Mfano
Hezekia aitawala miaka 29 Yerusalemu. Alifuata nyayo za mfalme Daudi. Aliondoa madhabahu zote za kuabudia miungu kwenye milima. Hata ile nyoka ya shaba aliiondoa, kwani watu wameanza kuiabudu:Akaivunja vipande vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani(m.4; maana ya jina hili ni “kipande cha shaba”). Na Mungu alikuwa pamoja naye, kwani Hezekia alishikamana naye katika yote. Aliwapiga Wafilisti na kuthubutu kukataa kumtumikia Mfalme wa Ashuru. Wakati Mungu alimpa mfalme huyo kuteka mji wa Samaria kwa sababu waliokaa hapohawakuitii sauti ya BWANA(m.12), alilinda mji wa Yerusalemu. Ni vema kumtegemea Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz