Tafakari Kuhusu HakiMfano
Kundi letu lilikaa karibu kwenye chumba nje ya kitengo cha wagonjwa mahututi. Upande mwingine wa chumba cha kusubiria hospitalini, mama yangu alikuwa akipata huduma muhimu.
Huenda ilikuwa ni wasiwasi wa kawaida tuliokuwa nao kuhusu mpendwa aliyekuwa akipambania maisha yake uliofanya mazungumzo kati yetu sisi wageni yawe mepesi. Mwana mama aliyekaa karibu nami alielezea hadithi kuhusu kukua katika familia kubwa ya ndugu saba. Kutoka kwa wote hao, ni yeye na dada yake mkubwa – aliyekuwa anapata huduma muhimu katika chumba kilichofuata – ndiyo walio hai. Licha ya vifo vyote alivyoshuhudia na majonzi aliyovumilia, hakuwahi kufikiria hata mara moja kwamba Mungu siye wa haki. Familia yake ilikuwa imepitia vifo vingi, lakini yeye aliamini Bwana ni mwenye haki. Katika hali ya hivyo, kifo kinatembelea familia ndogo vile vile.
Mara nyingi sisi hujiuliza kuhusu haki na usawa wa Mungu tunapofikia katika mazingira yaliyo zaidi ya udhibiti wetu, au yasiyopendeza katika hali yetu. Lakini Bwana ni mwenye haki naye atawala kwa usawa, wakati wote. Ni wakati tunaposema ‘Amina’ kwa ukweli huu tu ndipo tunapoweza kuona haki ya Mungu ikitenda kazi, hata katika nyakati zetu mbaya. Kupitia kwa ushuhuda wa mwanamke yule katika chumba cha kungojea, nilishuhudia utulivu wa kipekee ambao ni Roho Mtakatifu peke yake ndiye awezaye kutoa katika mazingira kama yale.
Changamoto: Je, kuna maswala ambayo ungependa kuachilia kuyadhibiti? Kumbuka kwamba Bwana ni mwenye haki wakati wote, mkabidhi wasiwasi wako yeye.
Maombi: Baba, ingawa ninaweza kuweka maswali kuhusu haki na usawa wako ninapoangalia dunia inayonizunguka mimi, inanikumbusha kwamba njia zako siku zote ziko juu zaidi ya zile za kwangu. Nisaidie niyaone maisha kupitia kwa jicho lako. Tafadhali niongoze katika yote niyafanyayo niwe mwenye haki na mwenye usawa unaofaa urithi wangu katika wewe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org