Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 7 YA 31

Kama watoto wa Mungu, ni wajibu wetu kutenda mema na kuleta nuru ulimwenguni. Tunaweza kusimama kwa haki na tukaleta tofauti katika maisha ya wale wanaokabiliana na ukosefu wa haki.

Katika jamii zetu, watu wanashughulika na kila aina ya ukosefu wa haki, kama vile ukatili wa nyumbani na unyanyasaji. Nafikiria kuhusu mwanamke mmoja mdogo, aliyekuwa anaishi katika kituo cha Jeshi la Wokovu baada ya kukabiliana na matendo mabaya kutoka kwa mumewe na shemeji zake. Aliyavumilia kwa sababu ya mtoto wake wa kiume. Kupitia kwa wema na neema ya Mungu, ameweza kuvuka na kuingia mahali pa furaha na salama. Wanawake wengi kama yeye wanakabiliana na changamoto majumbani na mahali pa kazi.

Vikwazo vya hali hatarishi na utamaduni mara nyingi huwasukuma wanawake gizani. Kama Wakristo, tunaweza kuwa nuru iletayo tumaini kwa wale walionyamazishwa. Ni muhimu kukumbuka kwamba haki na usawa vinatakiwa kusambazwa kwa wote, kama Yesu alivyoonyesha alipomwonea huruma mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi (Yohana 8:3-11). Hebu tupaze sauti zetu kwa ajili ya wasio na sauti na, kama taa mahali ilipowekwa, tuwaongoze kuelekea njia nzuri zaidi.

Changamoto: Unaweza kuwa umekutana na wanawake walio gizani wanaokabiliana na ukosefu wa haki na ukawapuuza. Je hivi sasa uko tayari? Kuwapa muda uwasikilize, uombe na ulete nuru maishani mwao.

Maombi:

Nataka, mpendwa Bwana, moyo uliochemka kwa ajili yako,

Moyo uliobatizwa kwa uwezo wa mbinguni;

Akili iliyo tayari, mkono ulio tayari

Kufanya chochote nikijuacho,

Kusambaza nuru yako kila ninapo kwenda.

(Salvation Army Song Book 497 v 3)

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org