Tafakari Kuhusu HakiMfano
Vifungu hivi vinazungumzia kiini cha haki, kilicho ndani ya huruma, na haki. Haki sio tu inahusu sheria na adhabu, inahusu kuwainua wanaokandamizwa, kusimama na waliotengwa na kuwatetea wale ambao hawawezi kuzungumza wenyewe.
Kama wafuasi wa Yesu, tunatakiwa kutafuta haki tukiwa na hamu dhahiri kuhusu lililo sahihi na la haki machoni pa Mungu. Inatupa changamoto tutafute kwa bidii haki kwa wote, tupambane dhidi ya ukosefu wa haki na ukandamizaji, na kujitahidi kuipata dunia ambayo haki na huruma vinadumu. Tunabeba mafundisho yake kuhusu haki, huruma na upendo katika yote tunayoyatenda.
Kuwa ‘maskini wa roho’ na tunaotambua mahitaji yetu ya neema na huruma ya Mungu inaangazia umuhimu wa kuiendea haki tukiwa na uvumilivu na huruma kwa wengine. Kwa kuongezea, njaa na kiu ya haki inasisitizia kutafuta kwa bidii kile ambacho ni sahihi na chenye usawa. Haki ya kweli inatokana na moyo mwaminifu na hutafuta kusimama na kanuni za Mungu za huruma, rehema na haki.
Changamoto: Soma Mathayo 5:3-12. Fikiria dunia ingefananaje kama tungeishi sawasawa na mawazo haya.
Maombi: Mpendwa Mungu, tujalie hekima ya kutambua ukosefu wa haki pale ulipo, ujasiri wa kuzungumza dhidi ya ukandamizaji na kwa huruma tusimame kwa ajili ya waliotengwa. Tusaidie tuwe na njaa na kiu ya haki, na tutende kwa haki katika yote tuyafanyayo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org