Tafakari Kuhusu HakiMfano
Wamebarikiwa namna gani wazazi wanaowafundisha watoto wao thamani ya upendo, huruma na haki. Wamebarikiwa namna gani watoto wanaokua wakitizama mifano hii nyumbani mwao!
Lakini zaidi ya hili, ni ya thamani namna gani kuwa na upendo wa ziada wa Mungu, ulio mpana kama anga, waenda juu kama mlima na waenda chini kama bahari! Mungu anatutaka sisi tuwe watetezi wa haki na upendo katika dunia hii iliyovunjika. Tunatakiwa kuwashirikisha wengine upendo huu.
Mercy Mathew alizaliwa katika familia tajiri ya Kikristo huko Kerala, kusini magharibi ya India. Alipofikia umri wa miaka 16, aliacha familia yake huko Kerala na akasafiri zaidi ya kilomita 2,000 kwenda kwenye nyumba ya watawa huko Bihar, mashariki ya India, akiwa na kusudi la kumtumikia Mungu. Haraka akatambua kwamba maisha kwenye nyumba ya watawa yalikuwa tofauti sana ukilinganisha na maisha ya watu wa kabila waliomzunguka, naye akaguswa na mateso yao. Kwa hiyo akaamua kumtumikia Mungu kwa kutumikia jamii za kabila katika India ya kati. Ili afanye kazi nao alibadilisha jina lake likawa Daya Bai na akavaa nguo za kikabila. Taratibu, katika miaka mingi, akaivaa desturi yao na mtindo wa maisha yao naye akakumbatiwa na jamii.
Sasa katika miaka yake ya themanini, Daya anasifiwa kwa jukumu muhimu la kuinua jamii za kabila zipate matunzo ya afya, elimu na vifaa vya kiuchumi. Ilikuwa ni mapambano yake ya maisha ya upendo dhidi ya ukosefu wa haki ambao makabila yalikuwa yanakabiliwa nayo kwa miongo mingi. Twaomba maneno yetu ya upendo na matendo yamdhihirishe Mungu wa kipekee kwenye jamii na kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanadamu wanaoteseka.
Changamoto: Katika majimbo ya India, vile vile na sehemu mbalimbali duniani, Wakristo kadhaa wanateseka kwa sababu ya dini. Fikiria kuhusu hali yako, na ujitoe kuleta umoja, maombi, kuwatembelea au kujibu mateso yao.
Maombi: Bwana, washa moto wa upendo wako usio na mwisho ndani ya mioyo yetu. Tafadhali tusaidie kuendeleza upendo wetu ili tuweze kuona maumivu ya kaka na dada zetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org