Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 12 YA 31

Mungu ni mahali salama kwa maskini na wasio na ulinzi, hasa wakati wa matatizo. Kati ya magumu na shida, unaweza kupata faraja, usalama na ulinzi katika Mungu. Bila kujali nini kitatokea, tunaweza kumwamini na kupata nguvu katika uwepo wake.

Kwa watu wengi, kukabiliana na wakati wa msongo wa mawazo na magumu inaweza kuwa kazi nzito. Wakati mwingine, kufahamu mahali pa kupata msaada katika mazingira ya shida inaweza kuwa vigumu. Hata hivyo, tunatiwa moyo kutafuta hifadhi kwake Mungu. Yeye ndiye chanzo cha upendo na rehema kisichopungua, ambaye siku zote atakuwepo hapo kwa ajili yetu tunapomhitaji, nasi tunaweza kupata amani na nguvu tunazohitaji ili tusonge mbele.

Mungu ni mlinzi kwa maskini na kwa wale wasio na ulinzi kwa sababu nyingine, kama kukandamizwa, kubaguliwa na magonjwa. Tutakabiliana na matatizo maishani, lakini tunaweza kuwa na uhakika wa kupata faraja na hifadhi katika Mungu wakati huo. Hatuna haja ya kukabliana na matatizo yetu peke yetu, lakini tunaweza kuamini wema na neema ya Muumba wetu. Badala ya kutegemea nguvu zetu kukabiliana na changamoto zinazotujia, tunaweza kuamini kwamba Mungu wakati wote atakuwa hifadhi na nguvu zetu.

Changamoto: Unawezaje kuwa hifadhi kwa wale wanaopitia wakati mgumu? Sote tunaweza kuwa vyombo mikononi mwa Mungu vya kutoa ulinzi na upendo kwa wale wanaohitaji. Kwa kuwa Mungu ni hitadhi yetu sisi, tunataka kuwa chanzo cha nguvu na matumaini kwa wale wanaotuzunguka.

Maombi: Bwana, tafadhali tusaidie tukwamini kwa sababu wewe ndiye nguvu na hifadhi yetu, na tafadhali tusaidie tuwe hifadhi kwa watu wanaopitia nyakati ngumu, kuwa vyombo mikononi mwako kuwapa ulinzi na upendo.

Andiko

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org