Tafakari Kuhusu HakiMfano
Naweza kutoa muhtasari wa kifungu cha Wagalatia 6:1-10 kwa maneno matatu: rehema, huruma na haki.
Kwa uzoefu wangu ndani ya Kanisa, nimetambua kwamba watu wageni wanapojiunga, huwa pana jitihada za makusudi za kuwasaidia na mahangaiko yao au kuwaongoza katika wokovu kupitia kwa msamaha. Hata hivyo, nimeshuhudia vile vile jinsi adui, katika mbinu zake, amesababisha hata viongozi wakubwa au waumini imara wa kanisa kujikwaa na kuanguka.
Hili kwa undani limenihuzunisha mimi, na hata zaidi kukatisha tamaa inaweza kuwa ni uhaba wa wale walio tayari kufanyia mazoezi Wagalatia 6:1: Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.’
Katika kifungu cha 9 na cha 10, Mungu anatuita tuwe wenye haki – sio katika hali ya kuhukumu, lakini katika njia ambayo inatafuta kuwarejesha wale ambao wamejikwaa. Tumeitwa kuwa wenye haki katika hali ambayo kama tumepokea msamaha kutoka kwa Bwana, tunatakiwa na sisi tusambaze msamaha pamoja na rehema, huruma na haki.
Changamoto: Tusishushwe mioyo au tusichoke kutenda mema, licha ya makosa ya wengine. Njiani, tutakutana na watu wanaojikwaa, lakini sisi lazima tukumbuke kumpenda mwenye dhambi huku tukichukia dhambi. Endelea kuiishi haki ya Bwana, na kwa wakati wake tutapokea zawadi za mbinguni.
Maombi: Mungu, tujalie mioyo iliyojaa upendo ili tuwe watu tunaowainua wengine juu. Tusisamehe wakati hisia zetu za haki za kibinadamu zinatupeleka kuhukumu. Twaomba hisia zetu za haki kutoka sasa na kuendelea zitoe sura yako, tukiwa tumejazwa huruma.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org