Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 16 YA 31

Isaya 58 ni sura inayohangaisha. Tunaona picha ya watu waliopofushwa na dhambi zao, huku wakiamini uongo ambao una uchungu moyoni. Kifungu cha 3, wanamlaumu Mungu kwa kukosa hisia kwa sadaka walizojibebesha wenyewe. Katika kujibu, Mungu alileta nuruni unafiki wao. Mungu awezaje kukubali sadaka yao wakati, huo huo, wanawakandamiza majirani zao!

Hata sadaka nzito na utumishi uliotukuka hautaweza kupata idhinisho la Mungu wakati inatolewa kufunika unyanyasaji na kulisha majivuno na kiburi. Historia imejawa na mifano ya wanaojiita Wakristo wanaotetea utumwa, unyanyasaji wa watoto na watu walio katika mazingira hatarishi huku wakitangaza nguvu za Kristo za kuokoa. Ni jambo la kujichanganya wenyewe namna gani!

Viifungu vya sita na saba vinabeba wale ambao tunaweza kuwafikia – wale wanaotufanyia kazi, ndugu zetu, wenye njaa, wasio na mahali pa kuishi. Mungu anapenda imani katika matendo – mzigo kufanywa mwepesi, kuondoa minyororo, kuwashirikisha wengine chakula chako, kuwapa wengine makazi, kuacha kujificha. Yakobo 1:27 inaita hii dini ‘safi isiyo na taka’. Hii ndiyo aina ya kufunga ambayo Mungu anaihitaji.

Changamoto: Watambue watu wachache wanaohitaji msaada katika jamii yako. Unaweza kuwa na nguo, pea za viatu au vitu vingine unavyoweza kutoa. Andaa begi la zawadi au boksi ili kufanya vitu vyako viwe vinavyoonekana zaidi. Kama una watu wanaokufanyia kazi, hakikisha hauwazidishii mizigo, walipe inavyostahili na kwa wakati.

Maombi: Baba wa Mbinguni, nifanye kuwa chombo cha haki kwa kuishi maisha ya upendo na utumishi kwa wanaokandamizwa na wanaonyanyaswa, wenye njaa na wasio na makazi. Naomba pasiwepo na kutofautiana katika kushughulika na wengine, pasiwepo na nia chafu, pasiwepo dhabihu ya bure, bali yote kwa kusudi na kwa utukufu wako. Amina.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org