Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 31 YA 31

Miaka mingi iliyopita, wakati mume wangu na mimi tulipotumika kama viongozi wa kanisa kijijini Afrika, tulisikia habari za msichana mtoto aliyekuwa aozwe na baba yake bila ya ridhaa yake. Msichana alikuwa na miaka 15, bado yuko shuleni, na hakufahamu haki zake katika mazingira hayo.

Nilijisikia kuwa hili wazi lilikuwa ni unyanyasaji na hakika ukosefu wa haki, lakini utamaduni na mazoea ya kijiji hayakulilaani swala hilo moja kwa moja. Lilikuwa eneo lenye kufifia, hata katika macho ya sheria. Nilimwomba Mungu anipe hekima, nguvu na mwongozo.

Niliamua kuchukua hatua hatarishi ili kuzuia ndoa hii, kwa hiyo tulimpeleka msichana polisi. Kesi yetu tukaikabidhi, nilitoa utetezi wa matendo yangu na kesi ikaamuliwa kwa upendeleo wetu. Serikali tayari ilikuwa inapambana na aina hii ya ukosefu wa haki katika nchi yetu na polisi walishukuru kwa kile tulichofanya kumwokoa na kumlinda msichana.

Naamini kwamba Mungu hutuandaa mapema kwa yale anayotuita tuyafanye. Tunapoingia katika utumishi, tunakuja kutambua kuna kazi nyingi zinazotakiwa kufanywa na wakati mwingine hatuna uhakika wa namna ya kukabiliana nazo. Lakini katika mambo yote, Roho Mtakatifu hutuwezesha na hekima kuu, nguvu na uelewa kwa jili ya kila kazi.

Changamoto: Wakati mwingine sisi huwa na shauku ya kubadili dunia kwa ishara kubwa, lakini hupuuza kufanya yale yaliyo rahisi: kuwapa chakula wenye njaa, kuwaoa maji wenye kiu, kuwakaribisha wageni, kuwatembelea wafungwa, kuwavika waliouchi, kuwajali wagonjwa, kuwafariji wenye huzuni. Simama hata angalau kwa ajili ya nafsi moja tu inayohitaji utumishi wako, upendo wako na kujali kwako kwa utukufu wa Mungu wetu.

Maombi: Baba mwenye Huruma, tunaomba nguvu zako tuwatumikie wale wanaohitaji upendo wetu. Twaomba tuwe na hisia kwa wale wanaotuzunguka na tujibu mahitaji yao kwa ujasiri. Roho Mtakatifu, tuwezeshe tuwatumikie wenye njaa, wanaokandamizwa na wanaotengwa. Amina.

Andiko

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org