Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 24 YA 31

Maneno haya yanatangaza kwamba Masihi ajaye amepakwa mafuta kuleta habari njema kwa maskini, kufunga mioyo ilivunjika, kutangaza uhuru kwa mateka na kuwachilia huru wafungwa kutoka gizani. Amri hii sasa imewekwa mikononi mwetu, watu wa Mungu!

Kama sauti za unabii, tuna heshima na wajibu wa kutembea pamoja na Mungu katika kuleta ufalme wake duniani kwa kuzungumza kweli, kuwathamini wasiothaminika na kuwaachia huru wale wanaokandamizwa.

Adui anafurahi kama sauti ya utume huu hutujaza na woga na mashaka, lakini ukweli ni kwamba Mungu mweza amekupaka mafuta wewe kwa ajili ya jukumu lililopo. Kupitia kwa Yesu, umepewa mamlaka ya kiroho kutembea katika Ufalme huu ukiita, na Neno lake linatuahidi sisi kwamba ‘Yule akuitaye ni mwaminifu, naye atatenda’ (1 Wathesalonike 5:24).

Changamoto: Nyamazisha kila mnong’ono wenye mashaka unaoweza kukuongoza uende mbali na mamlaka hii. Tegemea Neno la Mungu kukupa mamlaka na imani inayohitajika ili uwe mshindi katika utume huu. Uwe mshirika na Roho na upalilie maono yasiyotulia ya kuwaona wale ambao wamenaswa katika giza.

Maombi: Bwana, rejesha mioyo iliyovunjika kwa mikono yako ya uponyaji. Tutumie sisi kama vyombo vyako vilivyovunjika katika utume wako wa kuwatafuta waliopotea, na kuwaruhusu wanaoumia wapate mguso wa Mungu.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org