Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 25 YA 31

Ndugu mmoja anamuumiza mwingine. Mama mara moja anasema, ‘Mwambie ndugu yako samahani umekosea.’ Mtoto ananung’unika, ‘Samahani nimekosea’ bila kwa kweli kumaanisha hayo maneno, maneno yanasemwa kumfurahisha mama tu.

Tunaweza kufanya jambo lile lile na ibada yetu kwa Mungu. Tunakuja Kanisani Jumapili na kuimba nyimbo za kumsifu na kumpenda Mungu, lakini haturuhusu zitafsiri jinsi tunavyoishi kila siku. Katika Amosi 5:23, Mungu kwa uwazi anasema nyimbo zinazoimbwa kwa nia potovu ni kelele tu kwake.

Mungu hataki maneno matupu Jumapili, anapenda tuishi maisha yanayodhihirisha haki yake kila siku. Matarajio yake ni kwamba utaalamu wetu wa upendo kwake tuuishi kila siku katika maisha yetu sahihi na mienendo ya haki. Inatakiwa kuwa kama kijito kinachotiririka, kisichokoma, kinachofunika yote tuyafanyayo na tuyasemayo.

Changamoto: Tafuta nafasi kila siku, juma hili uonyeshe upendo wako kwa Mungu kwa jinsi unavyotenda na kujibu wengine. Wafunike kwa neema, rehema, na haki ya Mungu.

Maombi: Bwana, wewe ni Mungu wa haki. Hebu tusiseme tu kwamba tunakupenda, bali tuonyeshe kwa kuishi kwa haki na kutenda kwa haki kwa kila mmoja tunayekutana naye.

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org