Tafakari Kuhusu HakiMfano
Katika Matendo 4:32-34, tunaona picha ya waamini waliokuwa wamoja moyoni na akilini (tafsiri moja inatumia maneno ya (‘moyo’ na ‘nafsi’).
Kushirikishana hakukuwekwa juu yao na viongozi wa kanisa, bali kulikuwa na msingi wake ndani ya umoja wa roho na nafsi. Walipendana, wakatunzana na wakashirikishana walivyokuwa navyo na kila mmoja. Upendo uliokuwa unatiririka ndani ya jamii ya Wakristo ulitiririka hadi kwa jamii. Mpaka wakapata sifa ya ajabu ya kutunzana kuvuka utamaduni na wale ambao hawakuwa wanachama wa imani yao.
Naiona picha hii duniani kwetu katika kujieleza kwa kanisa., mahali kila mmoja huja pamoja na kuwashirikisha wengine kile alicho nacho. Iwe ana vingi au ana vichache kila mmoja huleta alicho nacho mezani. Hili hutokea kwa sababu ya upendo na neema ya Mungu kuwa yenye nguvu na ipo kazini katika maeneo yote haya.
Hii ni kutunzana sisi kwa sisi, kutoa sadaka binafsi ili kusaidiana, kufikiria ustawi wa kaka na dada Wakristo zaidi ya ustawi wetu wenyewe. Kuishi katika jamii ya aina hii ya amani hufanya iwezekane kuachilia hukumu, kuwatakia mema zaidi wale wote tunaokutana nao, na kuishi bila hofu au kukataliwa.
Namna hii ya kuishi inawezekana kwa sababu ya kujitoa kwa kawaida ili kuwa wa moyo mmoja na akili moja, kupenda kama Yesu, kushirikishana kila tulicho nacho, ili pasiwepo mtu mwenye mahitaji kati yetu.
Changamoto: Fikiria ‘wahitaji’ ni akina nani katika jamii yako. Una nini cha kushirikishana nao? Wanawezaje kujisikia wamejumuishwa? Tunawezaje kuwa wanaovuka utamaduni katika eneo letu la ushawishi na huduma?
Maombi: Bwana, naomba niwe na macho yanayoona ukosefu wa haki duniani wa wale walionavyo na wale wasionavyo. Naomba niwashirikishe vile nilivyonavyo wale wenye uhitaji, na sio tu waumini ‘kanisani’. Naomba niwe wa moyo mmoja na akili moja pamoja na waumini wenzangu na jamii zinazotuzunguka ili kuwaonyesha upendo, neema na rehema wale ambao wanauhitaji.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org