Tafakari Kuhusu HakiMfano
Ilivyorekodiwa katika Mithali kama hekima iliyopitishwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto, kifungu hiki ni mwito wa wazi wa kuishi kwa haki. Kutoka katika nafasi za upendeleo, tunaitwa tutumie sauti zetu tutetee haki. Katika Ufalme wa Mungu ulio juu chini, viongozi ni watumishi; wa kwanza anakuwa wa mwisho na wa mwisho anakuwa wa kwanza.
Hatuwezi kwa haki au kwa usahihi tukamtetea mtu au kikundi ambacho hatujachukua mda kukifahamu. Katika moyo wa Mithali 31:8-9 kuna maelekezo ya kuishi kwa mahusiano mmoja na mwingine, kuhusika kikamilifu katika maisha ya wengine kwa upendo na kuhusika Kikristo.
Upendo wa Kristo hutusukuma kuchukua hatua. Tunapowatetea wale ambao hawawezi kujitetea wenyewe – labda kwa sababu hawana jukwaa, ushawishi au uwezo wa kuongea – tunajenga Ufalme wa Mungu, sauti kwa sauti.
Changamoto: Fikiria ‘wasio na sauti’ katika jamii yako ni akina nani. Andika na tuma barua, barua pepe au kadi ya salamu kwao, labda waulize unaweza kuwasaidia namna gani kwa maombi na kwa matendo. Tulia usubiri kwa utulivu majibu yao.
Maombi: Bwana, naomba unipe masikio yanayowasikia maskini, niwe sauti inayozungumza kwa ujasiri dhidi ya ukosefu wa haki, na moyo unaokua katika upendo kwako na kwa wengine.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org