Tafakari Kuhusu HakiMfano
Tunawezaje kuchagua njia yetu tunapokabiliwa na maamuzi muhimu maishani?
Mara moja, sikuwa na uhakika kuhusu kuchagua njia yangu kwahiyo nilimhoji mwingine niliye mwamini. Niliamini nilitakiwa kutambua ni njia ipi ilikuwa sahihi au isiyo sahihi katika macho ya Mungu. Hata hivyo, walinifundisha kitu cha thamani: ‘Njia yoyote utakayoichagua, Mungu ataibariki. Chagua kwa ujasiri njia unayofikiri unaitiwa.’
Wakati mwingine utatakiwa kuchagua njia ambayo ni ngumu kwako. Vile vile zitakuwepo nyakati utafikiri upo katika njia sahihi, lakini wengine hawataweza kuelewa. Lakini Bwana wakati wote huwa wa kweli, na yeye ndiye anayeniongoza mimi kwenye njia sahihi.
Natamani kumwamini Bwana anayeniokoa mimi na kutembea moja kwa moja katika njia anayoniongoza.
Changamoto: Ukitafakari kuhusu maisha yako mpaka hapa, hebu tuandike chini jinsi chaguzi zilivyofanywa na baraka ulizopokea kama matokeo.
Maombi: Mungu, naamini utaongoza maisha yangu yafikie ubora, kwa hiyo nasalimu amri kwa kusudi lako. Naomba niwezeshwe kufuata njia unionyeshayo, hata nyakati za mashaka au za mambo magumu. Amina.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org