Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafakari Kuhusu HakiMfano

Tafakari Kuhusu Haki

SIKU 13 YA 31

Katika tamaduni nyingi, watoto wanaonekana kuwa hawana umuhimu na wanaonekana kuwa na umuhimu kidogo au hawana katika mfumo wa maisha ya jamii. Uwepo wao unachukuliwa kuwa vurugu, na shughuli zao zinaweza kusababisha usumbufu. Hata siku za Yesu, hii ilitokea wakati wanafunzi walipoona wazazi wakiwaleta watoto na, badala ya kuwakaribisha, waliwafukuza. Hata hivyo, Yesu hakuwakataa. Yesu aliwakumbatia na akaweka mikono yake juu yao, na akawabariki.

Kulingana na Marko 10:13-14, kuna fundisho muhimu kuhusu tunavyowatazama watoto kupitia kwa miwani ya Ufalme wa Mungu. Wanahusika, wanathaminiwa, wanapendwa, wanathamani vile vile kama watu wazima. Hizi ndizo thamani za Ufalme wa Mungu, kwa hiyo tunatakiwa kuonyesha haya katika maisha ya jamii yetu.

Watoto ni wenye thamani mbele za Mungu, na hii ni zawadi ambayo lazima tuikubali. Tunaamini kwamba hiki ndicho kizazi kinachofuata kitakacho endeleza kazi ya kutangaza habari njema ya Yesu Kristo, ili kizazi kijacho kiwe ni kile ambacho kinamheshimu Mungu.

Changamoto: Maisha yako yanaonyesha namna gani kwamba watoto ni wenye thamani na wanaopendwa na Bwana? Unaonaje thamani ya Ufalme wa Mungu ndani ya maisha yao?

Maombi: Baba yetu mpendwa, tujalie hekima tukue na kufundisha watoto wetu kulingana na maadili ya Ufalme wako. Twaomba watoto wetu wapate hekima ya Mungu katika maisha yao. Amina!

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org