Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

SIKU 11 YA 31

Injili hii ya Yohana iliandikwabaada yaPetro kuuawa! Petro alikuwa mfia dini. Aliuawa miaka 32 hivi baada ya Yesu kupaa Mbinguni. Simulizi moja la historia ya kanisa lasema kwamba alisulibishwa miguu ikiwa juu na kichwa chini! Ndivyo alivyotabiri Yesu:Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka. Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate(m.18-19). Petro alimfuata Yesu na kumkiri mpaka dakika ya mwisho! Hivyo alifanikiwa kutimiza ahadi ambayo mara ya kwanza alishindwa:Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako(Yn 13:37-38)! Unamjibuje Yesu akikuuliza:Wewe wanipenda kuliko hawa(m.15)?

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku / Oktoba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Oktoba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha