Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

SIKU 3 YA 28

Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu (m.18). Kabla Paulo hajaendelea kufundisha zaidi juu ya Injili anaonyesha jinsi Mataifa (1:18-32) na Wayahudi (2:1-3:20) wanavyopotea na kuhukumiwa na ghadhabu ya Mungu. Kuna makosa mawili ya msingi yanayomtenganisha Mmataifa na Mungu: 1. "Uasi", yaani kutokumwamini na kumtukuza Mungu. Kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza … (m.21-23). 2. "Uovu", yaani kufanya yasiyo haki. Hawa ni waipingao kweli kwa uovu (m.18). Je, uko chini ya ghadhabu ya Mungu?

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaid...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha