Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

SIKU 6 YA 28

Kwa sehemu Watanzania walimjua Mungu hata kabla wamisionari hawajaileta Injili. Kutokana na dhamiri zao waliweza kujua yaliyo mema na mabaya yaliyoandikwa mioyoni mwao (m.14-15). Na kutokana na uumbaji wa Mungu na matendo yake katika uumbaji waliweza kumtambua. Walijua yu mwema na kwamba huadhibu maovu kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia (1:19-20). Wabantu walimwita Mungu kwa majina mbalimbali, na baadhi ya mababu walimwamini kweli Mungu na kukataa maovu! Katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye (Mdo 10:3). Kwa uelewa zaidi linganisha na 10:1-5, Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaid...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha