Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

SIKU 5 YA 28

Maneno haya, wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria (m.12 na 17) yawalenga Wayahudi. Wengi wao walimkataa Kristo kwa sababu walikuwa wameambukizwa na unafiki wa Mafarisayo ambao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao (Mt 23:4). Mtu anaweza kwa mwenendo wake kuonekana mwema sana kuliko wale waliozungumziwa katika 1:18-32 ambao huipinga kweli kwa uovu na kubadili kweli ya Mungu kuwa uongo. Ila haitamsaidia lo lote ikiwa anayatenda hayo hayo kwa siri. Kwa moyo wake yuko mbali na Mungu. Mungu hana upendeleo. Hutafuta moyo ulio na toba ya kweli. Paulo anauliza, Waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? ... kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu (m.4-5). Je, una roho gani? Roho ya uasi na unafiki au roho ya toba?

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaid...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha