Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

SIKU 11 YA 28

Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria (m.28). Njia ya kufika kwa Mungu ni moja tu kwa watu wote, nayo ni imani. Imani ya kuamini neema ya Mungu kwamba bila ustahili wangu ananisamehe dhambi zote kwa sababu ya upatanisho katika kifo cha Yesu, ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake (m.25). Kwa kuamini haya twashinda katika kesi yetu mbele ya Mungu, twahesabiwa haki. Mungu ni hakimu na sisi ni washtakiwa. Anatoa hukumu kuwa hatuna dhambi, maana Yesu alipigwa na adhabu ya Mungu badala yetu!

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/