Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

SIKU 14 YA 28

Somo linaeleza ile imani ni ya namna gani ambayo ilimfanya Ibrahimu ahesabiwe haki! Pia twaambiwa ni imani gani inayotufanya sisi kushinda kesi yetu katika hukumu ya Mungu! Imani ya Ibrahimu ilikuwa imani ya kuamini ahadi ya Mungu, yaani ahadi ile ya kufanya jambo lisilowezekana kabisa kwa uwezo wa kibinadamu.Ibrahimu aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako (m.18)! Na sisi twahesabiwa haki na Mungu kwa imani hii ya kuamini ahadi ya Mungu, kuwa kwa kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo dhambi zetu zimeondolewa na mauti imeshindwa. Ni imani ambayo haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake; bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki (m.23-25)!

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/