Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

SIKU 12 YA 28

Hakuna njia ya mkato katika kushinda kesi yako mbele ya Mungu. Njia ya mkato ni kule kujisifia matendo yako mema mbele ya Mungu pamoja na kumwomba kwa neema yake akusamehe pale ulipokosa na kupungukiwa. Kwenye njia hii hakuna neema kabisa, kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu; lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni (m.2 na 4)! Ukitaka matendo yako yakusaidie kushinda kesi, ni lazima uwe mkamilifu kwa matendo, maneno na mawazo! Lakini huwezi! Bali ukitambua hali yako ya upotevu na kukubali kuamini kuwa Mungu anataka kukusamehe bure kwa neema tu, hapo umeokoka (rudia tena m.3 na 5-8)!

Andiko

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023

Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/