Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Kristo alitiwa mhuri kama Masiha na Mungu Baba (Yn 6:27,Mwana wa Adamu ... huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu). Kwenye msingi huu, waumini waliookolewa na Kristo wametiwa mhuri na Roho Mtakatifu (m.13,Nanyi pia katika huyo mmekwisha ... kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu). Wakati wa Paulo mhuri ulionyesha umiliki. Waumini ni mali ya Mungu. Mungu ametutia mhuri kwa kutupatia Roho wake ndani ya mioyo yetu kama dhamana (2 Kor 1:22,Naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu). Kama alama, kutiwa mhuri huu unamaanisha umiliki wa muumini na Mungu, na uhakika wa wokovu na urithi ule atakaoupokea siku ya ukombozi kamili (4:30,Yule Roho Mtakatifu wa Mungu ... kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi). Je, wewe umeshatiwa mhuri huu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/