Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 2 YA 28

Kila muumini amechaguliwa na Mungu kuwa mwanawe mpendwa (m.5,Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake). Dhambi ilitutenga na Mungu, lakini tayari alikuwa na mpango wa wokovu tangu milele. Huo ulikuwa umefichwa, lakini sasa Mungu ametufunulia, akiutekeleza katika Kristo Yesu. “Ukombozi” (m.7), maana yake ni kumtoa mtu kutoka katika utumwa fulani (dhambi) kwa malipo fulani (damu ya Yesu). Ni “masamaha ya dhambi” ambayo a) yanatuweka huru, b) kutuwezesha kufanana na Yesu ambaye ni mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi (Rum 8:29,Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi), c) kutufanya kuwa sifa ya utukufu wake (1:12,Katika [Kristo] tupate kuwa sifa ya utukufu wake), na kutenda mema (2:10,Tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo).

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/