BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Yesu anawafunza wafuasi wake waepuke unafiki wa viongozi wa dini. Wanazungumza kuhusu upendo wa Mungu lakini wanawapuuza maskini. Wanafahamu mengi lakini wanatumia tu ufahamu wao kupata sifa. Yesu analaani maisha haya vuguvugu na anafundisha kuwa Mungu anaona yote na kila mtu atatoa hesabu yake. Hili ni onyo na pia ni himizo. Ni onyo kwa sababu tamaa na masengenyo hatimaye vitafichuliwa. Wanafiki watajulikana. Ukweli utafunuliwa na maovu yatarekebishwa siku moja. Lakini pia ni himizo sababu Mungu haoni tu uovu wa wanadamu; anaona mema pia. Anaona mahitaji ya wanadamu na anajali viumbe wake. Yesu anawahakikishia wafuasi wake kuwa wakiutafuta Ufalme wa Mungu na kuutanguliza, watapokea hazina ya milele na kupokea yote wanayohitaji ulimwenguni. Bila shaka, hii haimaanishi kuwa maisha yatakuwa rahisi. Kwa hakika, Yesu anakubali kwamba wafuasi wake watapitia mateso. Lakini anaahidi kuwa watakaopitia mateso watamwona Mungu, na wanaotoa maisha yao ili kulitukuza jina lake watatukuzwa mbele za malaika. Kwa sababu ya hii, Yesu anawahimiza wafuasi wake kuamini kuwa Mungu atawapa wanayohitaji na anawaonya dhidi ya unafiki. Yesu anatamani watu wote wapokee mafundisho yake, lakini wengi wanayakataa.
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com