Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 15 YA 40

Katika sehemu hii ya kitabu cha Luka, Yesu amefikia mwisho wa safari yake ndefu kwenda Yerusalemu. Anawasili akiwa amebebwa kwenye punda kutoka Mlima wa Mizeituni kuelekea mjini. Njiani, umati unamkaribisha kama mfalme huku wakiimba, “Atukuzwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana.” Umati ulikumbuka kuwa manabii wa zamani wa Israeli walitabiri kuwa siku moja Mungu mwenyewe atawasili kuwakomboa watu wake na kutawala ulimwengu. Nabii Zakaria alitabiri kuhusu Mfalme atakayekuja na ataingia Yerusalemu akimwendesha mwana punda ili kuleta haki na amani. Umati unaimba kwa sababu unatambua kuwa Yesu ndiye ameleta matumaini haya yote.

Lakini sio watu wote wanakubali. Viongozi wa kidini wanachukulia utawala wa Yesu kuwa tishio kwa mamlaka yao na wanatafuta njia za kumshtaki kwa watawala. Yesu anafahamu yatakayotokea. Anajua kuwa Israeli haitamkubali kama Mfalme na kuwa kukataa kwao kutawaelekeza kwenye njia ya mauti na wataishia kuangamia. Hii inamfadhaisha. Na...inamghadhabisha. Anapoingia Yerusalemu, anaelekea hekaluni na kuwafukuza wafanya biashara wanaozuia utoaji dhabihu. Anasimama katikati ya hekalu na anawaambia, “hii ni nyumba ya sala, lakini mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.” Hapa anamnukuu nabii Yeremia, aliyesimama palepale, kituo cha dini na mamlaka ya kisiasa ya Israeli, na akawakosoa viongozi wa kale wa Israeli kwa njia ile ile.

Viongozi wa dini wanaelewa anachosema Yesu, lakini hawakubali. Na kama viongozi wa kale wa Israeli waliopanga njama ya kumwangamiza Yeremia, nao pia wanapanga kumwangamiza Yesu. Ili kusimulia tabia ya viongozi wa Israeli, Yesu anaelezea fumbo kuhusu mmiliki wa shamba la mizabibu aliyelikodisha kisha akasafiri. Mmiliki anatuma watumishi kwenye shamba lake la mizabibu ili kuangalia mazao, lakini wakodishaji wanawapiga watumishi wale na kuwafukuza mikono mitupu. Kwa hivyo mmiliki anamtuma mwanawe kwenye shamba lake la mizabibu kwa matumaini kuwa watamheshimu, lakini wakodishaji wanaiona kama fursa ya kujinyakulia shamba lile la mizabibu kwa kumwangamiza mrithi. Wanampiga na kumuua. Katika simulizi hii, Yesu analinganisha wapangaji waovu wa shamba lile la mizabibu na viongozi wa kidini wa Israeli ambao mara kwa mara huwakataa manabii wote waliotumwa na Mungu na ambao sasa wanajiandaa kumuua mwana mpendwa wa Mungu. Yesu anafafanua kuwa viongozi wa kidini wanatenda makosa yaliyotendwa na baba zao na kuwa hamu yao ya kupata mamlaka zaidi itawapelekea kuangamia.

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com