BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Injili ya Luka inaishia na Yesu akiwa na wanafunzi wake wote wanashiriki chakula kwa mara nyingine. Kila mtu anashangazwa na mwili wake uliofufuka. Wanaona kuwa yeye bado ni mwanadamu, lakini pia ni mkuu zaidi ya mwanadamu. Amekufa na akafufuka akiwa na mwili mpya. Kisha Yesu anawaeleza habari hii ya kustaajabisha. Atawapa uwezo ule ule wa kiungu uliompa nguvu, ili waweze kwenda na kushiriki habari njema ya Ufalme wake na watu wengine. Baada ya haya, Luka anatueleza kuwa Yesu alipaa kwenda Mbinguni, ambako Wayahudi wanaamini kuwa kiti cha enzi cha Mungu kipo. Wafuasi wa Yesu wanaendelea kumwabudu Yesu. Wanarejea Yerusalemu na wanasubiria kwa furaha nguvu ya kiungu ambayo Yesu aliahidi. Kisha Luka anaendelea na simulizi hii katika barua yake inayofuata, kitabu cha Matendo ya Mitume. Ni kwenye kitabu hiki ambapo anaelezea similizi ya kusisimua kuhusu jinsi wafuasi wa Yesu walipokea nguvu za Mungu na kueneza habari njema ulimwenguni.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com