BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Luka ni mwandishi wa maelezo ya kwanza kabisa kuhusu maisha ya Yesu, kifo, kufufuka kwake, na kupaa kwake kwenda mbinguni. Tunaita maelezo haya, Injili ya Luka. Lakini ulijua kuwa Luka pia ana toleo la pili? Tunalijua kama kitabu cha Matendo ya Mitume. Linahusu kile ambacho Yesu aliyefufuka anaendelea kufanya na kufundisha kupitia Roho wake Mtakatifu anayefanya kazi kupitia watu wake baada ya yeye kupaa kwenda mbinguni.
Luka anaanza Matendo ya Mitume kwa mkutano baina ya wanafunzi na Yesu aliyefufuka. Kwa wiki kadhaa, Yesu anaendelea kuwafundisha kuhusu Ufalme wake wa juu chini na uumbaji mpya aliozindua kupitiakifo chake na kufufuka kwake. Wanafunzi wanataka kuenda na kushiriki mafundisho yake, lakini Yesu anawaambia wasubiri hadi wapokee aina mpya ya uwezo, ili waweze kuwa na kila wanachohitaji kuwa mashahidi waaminifu wa Ufalme wa Yesu. Anasema kwamba misheni yao itaanzia Yerusalemu, kisha kuenda hadi Uyahudi na Samaria, na kisha kutoka hapo hadi kwa mataifa yote.
Dhamira kuu na usanifu wa kitabu cha Matendo ya Mitume unajitokeza katika sura hii ya kufungua. Hii ni similizi kuhusu Yesu akiwaongoza watu wake kupitia Roho wake ili kuyaalika mataifa yote kuishi ndani ya mapenzi na uhuru wa Ufalme wake. Sura saba za kwanza zinaonyesha jinsi mwaliko utaanza kuenea ndani ya Yerusalemu. Sura nne zinazofuata zinapanga jinsi ujumbe unaenea kwa wasio Wayahudi walio katika maeneo yaliyo karibu na Uyahudi na Samaria. Na kuanzia sura ya 13 kuendelea, Luka anatuambia jinsi habari njema za Ufalme wa Yesu zinaanza kufikia mataifa yote ya ulimwengu.
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com