Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 40 YA 40

Njiani kuelekea Rumi, mashua iliyokuwa imembeba Paulo inakumbwa na dhoruba kali. Kila mtu aliye humo anahofia maisha yake, isipokuwa Paulo aliye chini ya meli akishiriki chakula kama vile Yesu alivyofanya usiku kabla ya kushtakiwa kwake. Paulo anabariki na kuumega mkate, akiahidi kuwa Mungu yuko nao katika dhoruba. Siku inayofuata, mashua inaharibikia kwenye miamba na kila mtu anaelekezwa kwenye pwani akiwa salama. Wako salama, lakini Paulo bado amefungwa kwa minyororo. Anapelekwa Rumi na anawekwa chini ya kufungo cha nyumbani. Lakini hali si mbaya sana kwa sababu Paulo anaruhusiwa kukaribisha vikundi vikubwa vya Wayahudi na wasio Wayahudi ili kushiriki nao habari njema kuhusu Yesu, Mfalme aliyefufuka. Cha kushangaza, Ufalme wa Yesu unazidi kukua katikati ya kuteseka kwa mfungwa (Paulo) aliye ndani ya nchi ya Rumi. Ufalme wa Yesu ulio katikati mwa ufalme wenye nguvu zaidi ulimwenguni kwa wakati huo. Na kwa tofauti hizi kati ya falme, Luka anakamilisha maelezo yake kana kwamba ni sura moja tu katika similizi ndefu zaidi. Hapa Luka anawasilisha kuwa wasomaji wanapaswa kuelewa kwamba safari ya kushiriki habari njema haijaisha. Wote wanaomwamini Yesu wanaweza kushiriki katika Ufalme wake, unaoendelea kuenea hadi leo.

siku 39

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com