Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 34 YA 40

Luka anatuambia jinsi Paulo anapigwa mara kwa mara, kufungwa gerezani, au hata kufukuzwa kutoka kwenye majiji kwa kutangaza kuwa Yesu ndiye Masihi Mfalme wa Wayahudi na wa ulimwengu wote. Paulo anapofika Korinto, anatarajia kuteswa tena. Lakini Yesu anamfariji Paulo na kukutana naye katika maono usiku mmoja akisema, “Usiogope, endelea kuzungumza na usinyamaze. Niko na wewe. Hakuna atakayekushambulia wala kukuumiza, kwa sababu nina wengi katika jiji hili.” Na kwa hakika, Paulo anaweza kuishi katika jiji kwa mwaka mzima na nusu, akifundisha kutoka kwenye Maandiko habari za Yesu. Na watu wanapojaribu kumshambulia Paulo, kama Yesu alivyosema tu, hawafanikiwi. Kiongozi aliyejaribu kumuumiza Paulo anashambuliwa yeye badala yake. Paulo hafukuzwi kutoka Korinto, lakini katika wakati unaofaa, anaondoka jijini akiwa na marafiki wapya ili awatie nguvu wanafunzi waliokuwa wanaishi Kaisaria, Antiokia, Galatia, Frigia na Efeso.

Huko Efeso, Paulo anawatambulisha wafuasi wapya wa Yesu kwa zawadi ya Roho Mtakatifu, na anafundisha kwa miaka kadhaa, akikuza habari njema kuhusu Yesu kwa wote wanaoishi Asia. Huduma hiyo inastawi watu wengi wanavyoponywa kimiujiza na kuachiliwa huru, mpaka uchumi wa jiji unaanza kubadilika watu wanapoacha uchawi na kuacha sanamu zao ili kumfuata Yesu. Wafanyabiashara wa hapo ambao wanafaidika kutoka kwenye ibada ya sanamu wanakasirika na kuanza kuchochea umati wa watu kumtetea mungu wao wa kike na kupigana na wenzi wa kusafiri wa Paulo. Jiji linakanganyika, na ghasia hiyo inaendelea hadi karani wa mji anapozungumza.

siku 33siku 35

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com