BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Paulo anapofika Kaisaria, anashtakiwa mbele ya gavana, Felix. Paulo anajitetea, akishuhudia kuwa ana tumaini katika Mungu wa Israeli na anashiriki tumaini sawa la ufufuo na washitaki wake. Felix haoni sababu ya kumshutumu Paulo, lakini hajui cha kumfanyia pia, kwa hivyo anamtia kuzuizini bila sababu ya kisheria kwa miaka miwili. Wakati wote Paulo akiwa kizuizini, mke wa Felix anaomba kusikia kutoka kwa Paulo na Yesu. Felix anasikia pia na anaogopeshwa na matokeo ya Ufalme wa Yesu. Anaepuka mjadala huo lakini bado anamuita Paulo mara kwa mara akiwa na matumaini ya kupokea rushwa kutoka kwake. Hatimaye nafasi ya Felix inachukuliwa na Porkio Festo, na kesi ya Paulo inachunguzwa tena mbele ya Wayahudi ambao bado wanataka afe. Paulo anakana makosa tena, na Festo anamuuliza ikiwa yuko tayari kuhamisha kesi hadi Yerusalemu. Lakini Paulo hakubali na anakata rufaa ili kushitakiwa huko Rumi mbele ya Kaisari. Festo anaidhinisha ombi lake. Sasa kama Yesu alivyosema tu (Matendo ya Mitume 23:11), Paulo atatekeleza kusudi la Yesu ndani ya Rumi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com