BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Baada ya vurumai ndani ya Efeso kuisha, Paulo anaondoka na kurejea Yerusalemu kwa wakati kwa ajili ya sikukuu ya Pentekoste ya kila mwaka. Akiwa njiani, anatembelea majiji mengi ili kuhubiri habari njema na kuwatia moyo wafuasi wa Yesu. Katika hili, tunaona ulinganifu kati ya Paulo na huduma ya Yesu. Yesu pia alianza safari kwenda Yerusalemu kwa wakati kwa ajili ya sikukuu ya Wayahudi ya kila mwaka (kwa upande wake, Pasaka) na kutumia fursa ya kuhubiri habari njema ya Ufalme wake akiwa njiani. Na jinsi tu Yesu alivyofahamu kuwa msalaba ulikuwa unamsubiri, Paulo pia anajua kuwa shida na huzuni vinamsubiri katika jiji kuu. Kwa hivyo akiwa na maarifa haya, anapanga mkutano wa kuaga. Anawaalika wachungaji kutoka Efeso kukutana naye katika jiji lililo karibu, ambapo anawaonya kuwa mambo yatakuwa magumu zaidi atakapokuwa hayupo. Anawaambia wanafaa kuwa makini ili kuwasadia maskini kwa ukarimu na kulinda na kukuza makanisa yao kwa bidii. Kila mtu anahuzunika kwa kulazimika kumuaga Paulo. Wanalia, wanamkumbatia na kumbusu, na kukataa kuondoka kando yake hadi anapopanda meli yake inayoondoka.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com