BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Luka anaendelea kutuambia kuhusu safari za kimishonari za Paulo katika Ufalme wa Kirumi. Anavyosafiri, anashiriki habari njema kwa ujasiri kuhusu Ufalme wa Yesu na wengi wanasikia ujumbe wa Paulo kama tishio juu ya namna wanavyoishi kwa kufuata tamaduni za Kirumi. Lakini kuna wengine ambao hatimaye wanatambua ujumbe wa Paulo kama habari njema ambazo zinaelekeza kwa njia mpya kabisa ya maisha. Kwa mfano, Luka anatuambia kuhusu mlinzi wa jela kutoka Filipi. Tunakutana na yeye tunapofuatilia simulizi ya kufungwa kimakosa kwa Paulo na Sila.
Baada ya kushutumiwa kusababisha mkanganyiko jiji zima, Paulo na mfanyakazi mwenzake Sila wanapigwa na kufungwa gerezani. Huku wakiwa macho katika seli yao, wakiwa na majeraha, wanaanza kuomba na kumuimbia Mungu. Wafungwa wanasikiliza nyimbo zao za kuabudu wakati tetemeko kubwa la ardhi linatetemesha misingi ya gereza kwa nguvu hadi minyororo ya wafungwa inavunjika na milango yote ya gereza inafunguka. Mlinzi wa gereza anaona hili na kujua kuwa atauawa kwa kuwaacha wafungwa watoroke, na kwa kukata tamaa katika maisha, anataka kujiua kwa upanga wake. Lakini Paulo anamkomesha kwa wakati na kuokoa maisha yake. Kutokana na hili, mlinzi mkali wa gereza anakuwa mtulivu na kuanguka miguuni mwa Paulo na Sila. Anatambua kuwa maisha yake pia yanahitaji kuokolewa milele, na anataka kujua njia. Paulo na Sila wana hamu kubwa ya kuongea naye, na siku hiyo hiyo mlinzi huyo wa gereza na familia yake yote inaanza kumfuata Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com