BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Ujumbe wa Ufalme unaenea kote Yerusalemu, na idadi ya wanafunzi inaendelea kukua. Viongozi wanahitajika, hivyo mwanaume anayeitwa Stefano anajitolea kuwahudumia maskini ili mitume waendelee kutangaza ujumbe wa Yesu. Stefano anaonyesha uwezo wa Ufalme wa Mungu, na makuhani wengi wa Kiyahudi wanaamini na kuanza kumfuata Yesu. Lakini bado kuna wengi wanaompinga na kubishana na Stefano. Hawawezi kudhibiti busara ya majibu ya Stefano, kwa hivyo wanatafuta mashahidi wa uongo kumshutumu kwa kutomheshimu Musa na kutishia hekalu.
Ili kujibu hilo, Stefano anatoa hotuba thabiti inayosimulia upya simulizi ya Agano la Kale kuonyesha jinsi unyanyasaji wao kwake unavyofuata mkondo unaotabirika. Anaangazia wahusika kama Yusufu na Musa, watu ambao walikataliwa na kuteswa na watu wao wenyewe. Israeli imekuwa ikikataa wawakilishi wa Mungu kwa karne nyingi, na hivyo si jambo la kushangaza kuwa sasa wanamkataa Stefano. Wanaposikia hili, viongozi wa dini wanashikwa na ghadhabu. Wanamfukuza jijini na kuchukua mawe ili kumpiga hadi afe. Stefano anapoendelea kupigwa mfululizo kwa mawe, anajitoa kwa dhati kwake Bwana Yesu, ambaye pia aliteseka kwa sababu ya dhambi za wengine. Stefano anakuwa wa kwanza kati ya wafiadini wengi anapolia akisema, "Bwana, usiwahesabie dhambi hii."
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com