Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 27 YA 40

Katika sehemu hii, Luka anamtambulisha jemadari wa Kirumi, aitwaye Kornelio, anayewakilisha kila kitu ambacho Wayahudi walichukia kuhusu utawala wa Warumi. Malaika anamjia Kornelio na kumwambia amuite mtu anayeitwa Petro, ambaye anaishi nyumbani kwa Simoni huko Yopa. Kornelio anapotuma wajumbe ili kufanya hilo, Petro yuko pale pale malaika alisema angekuwa, akishiriki katika ibada ya maombi ya Wayahudi. Ghafla anapata maono ya kushangaza. Katika maono, Mungu anamletea mkusanyiko wa wanyama ambao Wayahudi walikuwa wamekatazwa kula na kumwabia Petro, “kula hawa.” Petro anajibu, “Sijawahi kula kitu chochote kichafu.” Lakini Mungu anajibu, “vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.” Maono haya yanajirudia mara tatu na kumwacha Petro akiwa amekanganyika.

Petro anavyoendelea kutafakari maono, wajumbe wanawasili wakiwa na mwaliko kwa Petro wa kusafiri nao ili kutembelea nyumba ya Kornelio. Petro anaanza kuelewa maono aliyoona. Patro anajua kuwa kuenda nyumbani kwa mtu asiye Myahudi kungehatarisha taratibu za ibada, hivyo kwa kawaida angekataa mwaliko. Lakini kupitia maono, Mungu alikuwa anamsaidia Petro kuona kuwa hafai kuita mtu yeyote mchafu; Mungu ana uwezo wa kufanya safi watu wote wanaomtegemea Yesu. Hivyo bila kupinga, Petro anaenda nyumbani kwa Kornelio na kushiriki habari njema kuhusu Yesu––kifo chake, kufufuka kwake na msamaha kwa wote wanaomwamini. Huku Petro akiendelea kuongea, Roho Mtakatifu anamjaza Kornelio na watu wote wa familia yake, kama tu alivyowafanyia wafuasi wa Kiyahudi wa Yesu katika siku ya Pentekoste! Vuguvugu linakua na kuwafikia watu wote, jinsi tu Yesu alivyosema ingefanyika.

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com