Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 30 YA 40

Baada ya Paulo na Barnaba kufukuzwa kutoka Antiokia, wanasafiri hadi jiji la Ikoniamu wakiwa na habari njema kuhusu Ufalme wa Yesu. Baadhi wanaamini ujumbe wao, lakini wale wanaoukataa wanaanzisha vurugu dhidi yao. Mambo yanakuwa magumu hadi jiji zima linagawanyika kuhusu suala hilo. Na wanafunzi wanapojua kuhusu matishio ya kifo dhidi yao, wanaenda majiji ya Likaonia, Listra, Derbe, na maeneo ya karibu.

Wakiwa Listra, Paulo anakutana na mwanaume ambaye alikuwa hajawahi kutembea. Paulo anapomponya kwa nguvu za Yesu, watu wanafikiri kimakosa kuwa Paulo ni mungu wa Kigiriki aliyekuja kuwatembelea, hivyo wanajaribu kumwabudu. Paulo na Barnaba wanawakosoa watu kwa haraka, wakisisitiza kuwa kuna Mungu mmoja tu wa kweli na wao ni watumishi wake. Lakini watu hawaelewi kabisa, na wanashawishiwa haraka na maadui wa Paulo na Barnaba kuwa badala yake wanafaa kumuua Paulo. Wanampiga Paulo kwa mawe hadi anapoteza fahamu. Wanachukulia kuwa amekufa na kuuacha mwili wake nje ya Listra. Marafiki wa Paulo wanamzunguka na wanashangazwa wanapomtazama akisimama na kutembea akirejea jijini. Siku inayofuata, Paulo na Barnaba wanatembelea Derbe ili kuhubiri Injili na wanarudi Listra na majiji ya karibu ili kuteua viongozi wa zaida kwenye kila kanisa jipya na kuwatia moyo Wakristo kuvumilia katika shida.

Andiko

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com