Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 23 YA 40

Katika sura za tatu na nne, Luka anatuonyesha jinsi uwezo wa Roho wa Mungu unavyowabadilisha wafuasi wa Yesu kabisa ili kushiriki Ufalme kwa ujasiri. Anaanza kwa simulizi inayowahusu wanafunzi wa Yesu, Petro na Yohana, ambao wanamponya mwanaume aliyepooza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wanaona muujiza huu wanashangazwa na kuanza kumtazama Petro kana kwamba alifanya hilo kwa uwezo wake mwenyewe. Lakini Petro anauambia umati umsifie Yesu tu kwa muujiza huu na kuwasihi washiriki jinsi Yesu alivyokufa na kufufuka tena kwa ajili ya kurejeshwa kwa watu wote waliopotea.

Petro anajua kwamba watu waliokuwa hekaluni ndio waliomuua Yesu, hivyo anachukua fursa hiyo kuwaalika kubadilisha mawazo yao kuhusu Yesu na kusamehewa dhambi. Kutokana na ujumbe huo, maelfu wanaamini ujumbe wa Petro na kuanza kumfuata Yesu. Lakini sio kila mtu. Viongozi wa dini wanakasirika mno wanapoona kuwa Petro anahubiri na kuponya katika jina la Yesu, hivyo wanawakamata Petro na Yohana papo hapo. Viongozi wa dini wanadai Petro na Yohana watoe maelezo ya jinsi mwanaume mlemavu aliyeponywa alivyoanza kutembea, na Roho Mtakatifu anamwezesha Petro kujibu na kueleza jinsi Yesu ndilo jina pekee linaloweza kuwaokoa. Viongozi wa dini wanachanganyikiwa wanaposikiliza ujumbe wa ujasiri wa Petro na kuchukizwa na ushupavu wa Yohana. Wanaona jinsi Petro na Yohana walivyobadilika kwa sababu ya Yesu, na hawawezi kukataa muujiza uliofanywa.

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com