Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 22 YA 40

Baada ya Yesu kutawazwa mbinguni, Luka anatuambia kuwa wanafunzi wako pamoja katika siku ya Pentekoste. Hii ni sikukuu ya kale ya Waisraeli ya kila mwaka, ambapo maelfu ya mahujaji wa Kiyahudi walisafiri hadi Yerusalemu ili kusherehekea. Wakati wa tukio hilo, wanafunzi wa Yesu walikuwa wakiomba, kisha sauti ya upepo mkali ilijaza chumba walichokuwepo kwa ghafla na ndimi za moto zikawa juu ya kichwa cha kila mmoja wao. Je, taswira hii ya ajabu inahusu nini?

Hapa, Luka anaangazia dhamira iliyorudiwa ya Agano la Kale ambapo uwepo wa Mungu unaonekana kama moto. Kwa mfano, Mungu alipofanya agano na Israeli katika Mlima wa Sinai, uwepo wake ulionekana kama ndimi za moto kileleni mwa mlima (Kutoka 19:17-18). Pia, uwepo wa Mungu ulijitokeza kama nguzo ya moto alipojaza hema ili kukaa miongoni mwa wana wa Israeli (Hesabu 9:15). Ila tu wakati huu, moto unatawanyika kuwa ndimi nyingi za moto juu ya watu wengi, badala ya kuonekana katika nguzo moja juu ya mlima au jengo. Hili linawasilisha jambo la kushangaza. Wanafunzi wanakuwa hekalu jipya linalotoka katika eneo moja hadi lingine ambako Mungu anaweza kukaa na kushiriki habari zake njema.

Uwepo wa Mungu haujazuiwa tena katika eneo moja. Sasa unaweza kuishi ndani ya binadamu wanaomtegemea Yesu. Luka anatuambia kuwa punde tu wafuasi wa Yesu walipopokea moto wa Mungu, walianza kuongea habari njema kuhusu Ufalme wa Yesu katika lugha ambazo hawakufahamu hapo awali. Mahujaji wa Kiyahudi wanashangaa kuwa wanaweza kuwaelewa wanafunzi wa Yesu kikamilifu. Bado Mungu hajakata tamaa kuhusu mpango wake wa kushirikiana na Israeli ili kubariki mataifa yote. Na katika wakati unaofaa tu, katika Pentekoste, siku ambayo wawakilishi kutoka kwa makabila yote ya Israeli wanarejea Yerusalemu, anatuma Roho wake ili kutangaza habari njema za Mfalme wa Israeli, Yesu ailiyesulubiwa na kufufuka. Maelfu walisikia ujumbe huu kwa lugha zao asili na wakaanza kumfuata Yesu siku hiyo hiyo.

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com