BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Yesu anaposubiri sherehe ya Pasaka akiwa Yerusalemu, anafundisha kila siku hekaluni kuhusu Ufalme wa Mungu na mambo yatakayofanyika baadaye. Wakati mmoja, Yesu anatazama na kuwaona matajiri wengi wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina ya hekalu na mjane mmoja maskini anatia mle ndani senti mbili pekee. Yesu anajua kuwa matajiri hao walitoa kutokana na wingi wa mali yao, bali mjane alitoa vyote alivyokuwa navyo. Kwa hivyo anazungumza na kuwaeleza wote wanaomsikiza, “huyu mjane maskini ametoa zaidi kuliko wote.”
Yesu sio kama wafalme wengine wanaothamini matajiri kwa sababu ya misaada yao mikubwa. Katika Ufalme wake, watu hawahitaji kuwa na mali nyingi ili waweze kutoa zaidi. Yesu anafundisha kuwa utajiri wa ulimwengu huu utakwisha na kwamba Ufalme wake umekaribia, kwa hivyo anawaambia wafuasi wake waepushe mioyo yao na wasiwasi na mali ya ulimwengu na badala yake wamtegemee yeye (kifungu cha 21:13-19, 34-36).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com