Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 14 YA 40

Kwenye sehemu hii inayofuata ya kitabu cha Luka, Yesu anawaponya vipofu na anazidi kutoa mafundisho ya kiroho kuhusu maana ya kuishi katika Ufalme wa Mungu ulio wa kipekee. Lakini kabla ya mtu yeyote kuanza kuishi maisha ya Ufalme kwa kuomba na kuonyesha ukarimu kwa maskini, sharti kwanza aingie. Hakuna anayeweza kuingia kwenye Ufalme wa Mungu isipokuwa kwanza anyenyekee na amtegemee Mungu kwa mambo yote. Wengine wanajitegemea na hawaelewi hili, hivyo anawaeleza fumbo hili. Asimulia kama ifuatavyo.

Siku moja, watu wawili wanakwenda hekaluni kuomba. Mmoja ni Mfarisayo, anayetambulika kwa ujuzi wake wa Maandiko na uongozi wake hekaluni, na wa pili ni mtoza ushuru, anayedharauliwa kuwa kibaraka mfisadi anayefanya kazi na Warumi. Mfarisayo anajiombea akisema jinsi alivyo mtakatifu zaidi kuliko watu wengine wote. Anamshukuru Mungu kwa hili. Lakini yule wa pili, mtoza ushuru, hata hawezi kutazama juu anapokuwa akiomba. Anapiga-piga kifua chake kwa huzuni na kusema, “Ee Mungu, nihurumie, mimi ni mwenye dhambi!” Yesu anamalizia simulizi yake kwa kusema kuwa mtoza ushuru ndiye pekee aliyekwenda nyumbani akiwa mkamilifu mbele za Mungu. Anafafanua jinsi hali hii ya kipekee inayostaajabisha inafanya kazi katika Ufalme wake: “Kila anayejiinua atashushwa, lakini anayenyenyekea atainuliwa.”

Luka anasisitiza mada hii ya unyenyekevu kwa kuzingatia mafundisho ya Yesu na tukio lingine katika maisha ya Yesu. Luka anafafanua jinsi katika tukio fulani, kina mama na baba waliwaleta watoto wao wachanga kwa Yesu ili awabariki. Wanafunzi wanaona kuwa huu ni usumbufu. Wanawakemea na wanajaribu kuwafukuza. Lakini Yesu anawatetea watoto kwa kusema, “Waacheni watoto waje kwangu, na msiwazuie, maana Ufalme wa Mungu ni wao.” Anamalizia kwa kutoa onyo na mwaliko huu, “Mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauona kamwe.”

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com