BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano
Yesu anapojiandaa kuelekea Yerusalemu, anawatuma wafuasi wake kwenda kuandaa kila mji ambako ananuia kupitia. Wanaondoka bila chochote, hawabebi mizigo wala mikoba ya pesa, na wanakwenda wakiwa na nguvu za kuponya pamoja na ujumbe kuhusu Ufalme wa Mungu. Hii inatuonyesha tena kuwa wafuasi wa Yesu ni watendakazi katika wito wa Mungu ulimwenguni. Yesu anahubiri habari njema ya Ufalme, na wanaoiamini hawaipokei tu, wanajiunga naye katika kuieneza kwa wengine. Hii ndiyo njia ya Ufalme. Sio kuhusu kupata mamlaka na utajiri wa ulimwengu huu; ni kuhusu kupokea baraka za mbinguni ili kubariki ulimwengu. Kwenye sehemu hii inayofuata, Luka anasimulia mafundisho ya Yesu kuhusu kumtegemea Mungu. Yesu anafundisha kuhusu kuomba, kutumia rasilimali ipasavyo na kuwa wakarimu. Mafundisho yake yanawapa furaha maskini na wanaoteseka. Lakini viongozi wa dini wanaghadhabishwa wanapomsikia Yesu akikosoa maisha yao ya tamaa, na wanaanza kupanga njama dhidi yake.
Kuhusu Mpango huu
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com