Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 9 YA 40

Vifungu vya leo vinaonyesha jambo la kustaajabisha kuhusu wito wa Yesu. Yesu anasema kuwa yeye ndiye Masihi (Kristo), ila anasema kuwa hatatawala Israeli kama alivyofanya mfalme mwingine yeyote aliyetangulia. Atatawala kama mtumishi mwenye kuteseka anayerejelewa kwenye kitabu cha Isaya sura ya 53. Atakufa ili kutwaa enzi yake. Kisha Luka anachambua upekee wa kisa kinachofuata.

Katika simulizi hii, Yesu anawapeleka baadhi ya wanafunzi wake mlimani, ambako uwepo tukufu wa Mungu unaonekana kama wingu linalong'aa. Naye Yesu anapewa mwili mpya. Watu wengine wawili wanajitokeza, Musa na Eliya, manabii wawili wa kale ambao pia utukufu wa Mungu uliwashukia mlimani. Mungu ananena kwenye wingu akisema, “Huyu ni mwanangu, msikilizeni.” Hili ni tukio la kustaajabisha! Kisha Luka anatueleza kuwa Yesu, Eliya na Musa wanavvyozungumza kuhusu kuondoka au “kutoka” kwa Yesu. Luka anatumia neno la Kigiriki exodos (neno linalotumiwa na Wagiriki kurejelea kifo) kama njia ya kuonyesha uhusiano kati ya atakalotenda Yesu mjini Yerusalemu, na kutoka kwa Waisraeli nchini Misri. Kwa hili, Luka anatuonyesha kuwa Yesu ndiye nabii mkuu zaidi. Yeye ndiye Musa wa kizazi kipya ambaye, kupitia kuondoka kwake (kifo), ataikomboa Israeli kutoka kwenye ufalme wa dhambi na maovu yote.

Na baada ya ufunuo huo wa kushangaza, huduma ya Yesu huko Galilaya inakamilika, kisha Luka anaanza simulizi kuhusu safari ndefu ya Yesu kuelekea mji mkuu ambako atakufa ili kutawazwa kuwa mfalme wa kweli wa Israeli.

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com