Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 30 YA 31

Kwa watu ambao wanapambana kila siku na msongo wa mawazo na wanaishi maisha yao kwenye lindi la kukata tamaa, ni muhimu kuelewa uhusiano kati ya furaha na shukurani. Kama wewe ni mtu mwenye shukurani, furaha haiko mbali na wewe. Kama ni mtu mwenye furaha, nakuhakikishia uhesabu baraka Zakayo kila siku na kwa sauti kubwa.
Shukurani ni ufunguo unaofungua mlango wa uwepo wake kwa watu wake. Na unapoingia kwenye uwepo wake, unajua kwa uhakika kwamba utapata furaha.
Kwa hiyo leo kama unasongwa na huzuni au kukata tamaa katika maisha, orodhesha vitu ambavyo unamshukuru Mungu kwavyo.
Ninaamini kwa mkristo, shukurani si za kuweka kwa ajili ya siku moja ya Mwaka au ya msimu tu. Shukurani lazima iwe ni mfumo wa maisha yako. Moyo wenye Shukurani ni mahali penye rutuba ambapo mbegu za furaha huota na kustawi kwa wingi.
siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com