Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 26 YA 31

Usidharau umuhimu wa utakatifu katika kusudio lako la kuwa mkristo mwenye kujawa na furaha. Kama unadhani unaweza kuishi maisha ya kuchangamana na dhambi na mbinafsi na bado ukawa mnufaika wa furaha ya mbinguni, jifikirie upya!

Biblia, kutoka Mwanzo mpaka Ufunuo, imejaa mashauri ya Mungu juu ya umuhimu wa kuishi maisha matakatifu. Sizungumzi habari za sheria au kifungo! Utakatifu ni wazo la Mungu wa uhuru na maisha katika ubira wake.

Utakatifu kwa lugha nyepesi ni kuishi kwa kufuata njia za Mungu. Inaweza kumaanisha kubadili jinsi ya unavyoongea au jinsi unavyotumia muda wako.

Leo, hebu angalia maisha yako na muombe akufunulie chochote katika maisha yako ambacho kinatakiwa kubadilishwa. Kama wazo linakujia kwamba umekuwa siyo mvumilivu kwa mwenzi wako, usidharau wazo hilo. Yawezekana linatoka kwa Mungu na anakuonesha eneo katka maisha yako linalotakiwa kubadilika!
siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com