Jolt ya FurahaMfano
Je, unajua kwamba umeshapewa kila kitu unachohitaji uli uishi maisha ya furaha? Mungu Baba, kupitia kwa Yesu mwanawe, ametupa kila kitu kwa ajili ya kuishi maisha ya utaua. Na kwa sababu furaha ni moja ya tabia za Mungu, inayojumuisha nguvu kamili na furaha kamili.
Unapokuwa na Yesu Kristo, tayari una kila kitu cha kuweza kushughulika na msongo wa mawazo, tabia ya kushutumu, kutokuwa na subira na kushindwa. Mungu ni mkarimu kuliko mtu yeyote wa sasa au aliyekuwepo, ametupa kila kitu tunacohitaji ili tuishi maisha ya utoshelevu na furaha.
Ni ahadi ya thamani sana tunayopata kuwa washiriki wa asili ya Mungu. Sisi si watu bandia wa dunia, lakini tuna fanana, tunatenda, tunaongea, tunatembea kumfanana Yesu alivyofanya akiwa duniani. Asili yeynyewe ya Mungu yaweza kubadili udhaifu wetu katika kila eneo la maisha yetu kama tutamruhusu yeye kufanya hivyo. Tunapotembea na kuishi katika roho, ni wazi tunatembea uelekeo tofauti na tabia zetu za asili.
Kama utatumia mistari hii katika maisha yako, utakuwa ni aina ya yanayowezekana kwako. Itachukua kazi ngumu? Ndiyo! Inatakiwa juhudi za dhati, lakini Mungu mwenyewe atakutia nguvu unapokuwa kama yeye kila siku ya maisha yako!

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.
More
Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com