Jolt ya FurahaMfano
Siyo sifa za mtu tuu , furaha ni ni zawadi ya uwepo wake. Unapomwomba Yesu aingie moyoni mwako na kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, furaha ya mbinguni hushuka na kukukumbatia kila siku ya maisha yako. Furaha inatokana na uwepo wa Mungu na haitokani na mazingira.
Unaweza kuwa na furaha hata kama maisha yako yanayumba kwa sababu Mungu ameahidi kuwa hatakuacha. Furaha haitakiwi kuja na kuondoka kama fedha au hali ya hewa! Furaha ni ya kudumu siku zote kwa sababu Mungu yupo nasi wakati wote.
Hakuna unachoweza kufanya, hakuna maneno unayoweza kusema, ambavyo vinaweza kukuondoa kwenye uwepo wake. Hakuna mahali ambapo unaweza kwenda ambapo utakuondolea ushirika wako na yeye. Yupo kila mahali na utajiri wa kujua kwamba yuko nawe siku zote.
Hakuna hata siku moja katika maisha yako ambayo hajawahi kuwa na wewe, akikufariji na kutamani uhusiano wako kwake. Furaha ni kujua kwamba yuko pamoja na wewe... kwenye siku nzuri na siku mbaya... nyakati za shukrani na siku za kukata tamaa. Furaha ya uwepo wake inakuzingira na kukulinda. Fahamu leo ni mwema na yuko pamoja na wewe. Hakuna furaha iliyo kuu kama hiyo!

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.
More
Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com